Friday, July 15, 2016

MAONESHO YA BIASHARA YA KIMATAIFA KWA A. MASHARIKI
 
Na Mjomba Remsi
Dar Es Salaam, 14 July 2016
Maonesho ya Biashara  ya Kimatifa – International Trade Exhibition yaliyodumu kwa siku mbili yamefikia ukomo leo, baada ya  washiriki wa kimataifa kuonesha bidhaa zao na vifaa vyao wakiwa wamelenga nchi tano (5) za Afrika ya Mashariki.
Maonesho hayo ya biashara yalikuwa na bidhaa mbali mbali zikiwa ni vifaa vya viwandani  na vifaa vya kilimo na madawa pamoja na mawasiliano – teknohama.
Mabara matatu yaliwakilishwa kwa uwazi kabisa ikiwa ni pamoja na makampuni ya kutoka Bara la Ulaya, kutoka Asia na Afrka. Hali kadhalika eneo la Eurasia lilipata uwakilishi katika maonesho hayo ambayo yalikuwepo Mlimani City, kuanzia Julai 13.
Katika maeneo yaliyoweza kuonekana kwa haraka haraka ni  vifaa  vya viwandani  kama vile  mashine za kutengenezea nyaya, mashine za kuchimba ardhi na kilimo- earth moving and agricultural equipments pamoja na mmitambo ya kuchapisha vitabu magazeti na vipeperushi.
Afrika Mashariki ina wakazi zaidi ya milioni 100 wakiwa wanaishi katika nchi za Burundi, Kenya, Rwanda , Tanzania na Uganda. Na Lugha kuu zinazotumika katika maeneo haya ni  Kiswahili ambacho kitumika katika nchio zote bila  mipaka, Kingereza  ambacho kimo kwa wingi katika nchi tatu zikiwa ni Kenya Uganda na Tanzania na Rwanda kidogo. Halafu lugha ya Kifaransa ambayo inatumika Burundi na Rwanda.
Wananchi wake wengi ni wakulima na hivyo  kwa makampuni yaliyoshiriki katika maonesho kuandaa maonesho ya bidhaa za kilimo na namna ya kutengeneza na kutayarisha mazao ndio hasa mahali pake.
Washiriki wengi ambao ni wageni walifurahi sana na kusema kuwa wamepata wageni- wapitaji kuangalia bidhaa na kuuliza  na kuweka maandaliizi ya mawasiliano pamoja na mikataba  walikuwa ni wengi.
Hata hivyo kuna makampuni mengine ambayo yalikuwa yako tayari kuingia ubia na makampuni ya hapa Afrika Mashariki  au kwa uchache kama wangelipata mawakala wao kwa bidhaa zao.

No comments:

Post a Comment