NZEGA, FAST GROWING TOWN AND SOON TO SURPASS TABORA
Mjomba Rems,
There was a
time, when somebody living anywhere in
Nzega District, after the afternoon said, I want to go to town. People would
ask him, By what means or do you use a
wungo? That was because mjini then was referred to Tabora only and every other
place in the area was Kijijini and those intending to go to Nzega would refer
to it as Wilayani.
After the
mines and many developments in communications, now Nzega has boomed up. It
needs to be a region of its own as the
town is so large just as Tabora town
was 30 years ago and the communications
are better than what Tabora town had in that time.
Nzega is a
hub of matters:
1.
It
is a hub of business as far as minerals
are concerned, you have every thing from zinc, lead to gold. Nsungangwanda is
part of it.
2.
In
transport, Nzega is not that backward.
The tarmac stretches from Nzega to Mwanza and of course straight it goes
through Ipuli to the Central Bus Stand
of Tabora at Kachoma.
3.
Political
Hub as that is the place where we had great politicians of Tanganyika and
Tanzania namely Kasella Bantu and others. Kasella Bantu is always remembered in
his case when he was the MP of the area
and cattle rustlers menaced the area and
he said, WINJAGI DOH!. ..meaning only remove them. And when the rustlers came again this time,
the villagers came with a village call named MWANO and the whole village fell
on them and crushed them to pulp. The Mp
was arrested in that case.
4.
Nzega
is Historical as that is where the name Mwaisela
Ward of Muhimbili comes from as there was a doctor of that name who lost
his life at Uchama area and he was a
famous person not only then and even now.
5.
And
on the other side Tabora seems to be at the dead end as the roads towards South
are hazardous, there are at signs along
Sikonge Road that show that you travel on your own risk as there is a sign of a human skull and leg bones just like the
flag of the PIRATES.
SIKONGE
Cheupe Nyati,
Katika
majina ya maeneo ya Mkoani Tabora, mengi yamekosewa lakini la Sikonge
limekosewa zaidi na kuna haja ya
kulisahihisha na kuleta usahihi wake
katika maandiko mbali na vitabu.
Hayo
yalisemwa na Mzee Mwana Kamwelwe, Ise wa Mbogo, akifafanua kuwa jina hilo
usahihi wake ni VIKONGE, na hiyo ikiwa na maana ya mikonge ambayo kwa jina jimgne ni katani.
Mzee Mbogo
ambaye anaishi maeneo mjini Sikonge
anasema mpaka hivi leo watu wakizungumza kwa Kinyamwezi hawatamki
Sikonge bali, mtu anasema “Naya Vikonge “ maana yake “Nakwenda Vikonge”.
Akielezea
asili ya neno hilo alisema kuwa eneo la wilaya hiyo lina mimea hiyo ambayo
Wanyamwezi wanaiita “makonge” na yako mengi. Yanapatikana karibu katika kila
kisuguu.
“ Tangu
zamani tulikuwa tukichukua mimea hiyo na kuichuna na kupata nyuzi zake ambazo
ni nyeupe kabisa na tunasokota na kupata kamba kwa kazi nyingi tu”, alisema
Mzee Mbogo.
Akielezea
kuwa akasema kuwa kamba hizo zilitumika kusokota kamba nyembamba na kamba
kubwa kabisakama ifuatavyo:
1.
Kapwe- ni kamba nyembamba ambazo hutumika
kwa kutegea ndege wadogo wadogo kuanzia
jorowe, tetere (njiwa mwitu), huwa tutu (mapula), kwale na makanga.
2.
Ipwe- ni kamba ambayo ilitumika kwa
mitego mikubwa kwa ajili ya wanyama wakiwemopaa, nyemela na wanyama wengine wengine ambao umbo lao
halizidi kimo cha mbuzi.
3.
Ngwisi – kamba ambayo ilitumika kufungia
mbuzi, kondo na ng’ombe wakati wa
kuwakamua maziwa ng’ombe anafungwa miguu
yake na wakati wa kulima kamba hiyo inazungushwa kwenye pembe. Unene wa kamba
hii Unaweza kuwa kama dole gumba au kama dole gumba la mguuni kulingana na haja
ya kazi.
4. Igalavwa - Ni kamba ambayo unene unazidi dole gumba la mguuni nampaka kuwa na
ukubwa wa mkono. Matumizi yake ni mengi
sana lakini tusheke tu na kusema kuna matumizi ya:
a)
Kwa
ajili ya shughuli za kutunduka na kushusha mizinga ya asali (nyuki).
b)
Hutumika
kwa kazi za ujenzi na shughuli za kupasua mbao.
c)
Kamba
kama hiyo ikitumika katika michezo ya kuvutana- Kavwivulule/Tug of war
Aina ya kamba iliyotengenezwa kwa kutumia nyuzio za katani ikiwa
imetumika kwa kusuka kutumia minyororo mitatu. Aina nyingine ni kwa kusokota kwa
kutumia minyororo miwili
Kwa kusisitiza kuwa jina hilo linatakiwa kubadilishwa Mzee Mbogo alisema kuwa hiyo katani iliyotoka huko Marekani imetokea mahali panapo itwa Yukatan na hilo jina halikubadilika kwa nini jina la VIKONGE libadilike, je ni kwa sababu watu wanashindwa kusema Vi au inashindwa kuandikika.
Mbona Landani hawaiandiki wenyewe kuwa ni Landani wakati wanaandika ni London na wanajua vipi wanatamka lakini na sisi shauri zao watamke namna watakavyo lakini jina letu libaki Vikonge. Alisema kwa kusistiza.
Akitaja neema za Wilayani Vikonge Mzee alisema kuwa kulikuwa na Hospitali ambayo ilikuwa inajulikana nchi ya Tanganyika nzima na ambayo ilikuwa pale mahali panaitwa Misioni, “Bado ipo. Lakini wapi Madaktari? Nani atamfikia Daktari akiitwa Kiveli? We acha tu.”
Aina ya Mkonge unaopatikana katika
aina mbali mbali za mbuga za Sikonge/Vikonge
Wilaya saba (7) za mkoani Tabora na Wilaya ya Vikonge ikiwa
katika rangi nyekundu
Ambazo sasa zinatengenezwa kama mauwa
kwa ajili ya mapambo ya nyumbani. ( Picha na iita8860)
Aina
nyengine ya mkonge ambao unapatikana katika nyika za Sikonge/Vikonge
Ikiwa Ndiyo
mimea ambayo Ndiyo asili ya sehemu hiyo kuitwa Vikonge kutokana na
Vikonge
hivyo (picha kwa hisani ya internet)
No comments:
Post a Comment