Na Cheupe Nyati in Prague
Katika
mazungumzo na watu ambao wametembea hasa katika mipaka ya nchi za maziwa makuu.
Nchi ambayo
inaogopwa sana ni Kongo. Kongo hakuna wizi, kongo hakuna utapeli, kongo kuna mambo mengi sana.
Lakini kwa
leo hii nakwambia kuwa nilipata habari wakati
nikisoma nje ya nchi – overseas, basi tulikuwa na kijiwe sisi watoto
ambao tunaozungumza Kiswahili.
Walikuweko:
1. Wakongo
2. Warundi
3. Wanyarwanda
4. Wakenya
5. Wabonngo
6. Na
waganda
Katika visa
vilivyokuwa vinatolewa ilikuwa ni mtu
anaweza kueleza ama yale aliyaona au yale ambayo anaona kuwa ndiyo mila na
tabia za kwao.
Huyu mtu
ambaye alikuwa ni Mkongo , lakini alikuwa na nyaraka za safari za Kibongo
kamili kabisa. Alisema kuwa pamoja na kuwa pasi hiyo aliipata Tabora, Tabora siyo asili yake bali yeye alitokeya
Kivuu.
Anaeleza
pamoja na mambo mengine yaliyokuwa si usalama kwake huko mpaka akakimbia akiwa
na miaka kama saba au minane ni kukwepa
mauaji ya Pierre Mulele ya Mayimayi.
Kubwa zaidi
ni kuwa yeye alikuwa amezaliwa pacha na mweziwe. Katika maisha yao kabla hata
hawajaanza kwenda shule alikuwa
anaona watu wanafanya mambo ambayo
alikuwa hayaelewi. Mtu akiugua basi
kabla muda haujapita mrefu anasika kimya huyo mtu hayupo na wala watu hawasemi
kitu juu yake.
Siku
moja akaona babu yake ambaye alikuwa anaitwa
Muzee Mayuto ameletewa mzigo umefungwa na majani ya mugomba. Yeye aliwaambia
wapeleke huo mzigo huko chumba cha ndani. Walipita na madamu yalikuwa yana vuja
. Ah hao mabwana waliingi humo ndani na kutua mzigo wao wakatoka . Muzee Mayuto
akauliza mzigo umetoka wapi huo? Wale watu wakasema Yule ni mutoto wa Muzee
Kasembe kule kwa upande wa ng’ambo ya muto.
Muzee Mayuto akasema mbona gafla hivyo na alimuona kule
kwenye arusi ya Kitwana enga mbili zilizopita. Ah weye muzee hizo ndizo salamu za Muzee
Kasembe hawezi kukusahau wewe rafiki wake mpendwa. Boh
Inga ile
ilipita na sisi tulikuwa tunafurahi kuwa na mchuzi mule kwetu. Lakini Yule
ndugu wangu pacha alishikwa na homa kali sana
na akawa ana tetemeka. Mara wakaja wale watu walioleta salamu kutoka kwa
Muzee kasembe wakasema wanamuliza Muzee
Mayuto, “Muzee Kasembe anauliza vipi
hakuna salamu zozote maana
kachoka kula ugali na sombe anataka apate kamchuzi kidogo.” Muzee Mayuto
akasema apana hamuna kitu. Wale wajumbe wakasema mbona wamesikia kuwa humo kwake mambo tayari yeye anangoja tu , lakini usimusahau
kamchuzi.. sisi tunakwenda “
Wale watu
walikwenda na huku nyuma nikamuliza babu
kuwa wale walikuwa kina nani na walikuwa wanatafuta nini mbona salamu
zao hazifahamiki…. Babu alicheka sana akasema , “Ah na weneye mguruguru
sana hebu tiondokeye hapa”.
Kwa kuwa
ndugu yangu alikuwa yumo ndani mimi
nichukua manati yangu na kuingia msituni nikawinde ndege. Nilifika huko
nikapotea njia mpaka usiku ukaingia na mara kwa bahati tu na mwezi ulikuwepo
nikatokezea nyumbani.
Nikakuta
watu wamekoka moto na wanaota hapo usiku, lakini palikuwa kimya na hakuna mtu anayesema kitu. Mara nikaona
watu wanatoka ndani na mizigo ya vitu vimefungwa kwa majani ya migomba , hao
wanatoka na wanakwenda ; Walipotoka Muzee Mayuto akasema mupeni salamu zake
Kasembe, lakini kalikuwa bado kadogo
aniwie radhi… tunaonana siku nyingine.
Ehe
jamani kumbe Yule pacha wangu amekwisha
kufa na watu wamemchaanga na kupeleka zawadi kwa jamaa zake Muzee Mayuto.
Lakini sisi mule ndani ni mwiko na mwiko kabisa kula muchuzi wa mtoto wa mule
ndani.
Aa ah! Kumbe
! sana nifanye nini miye Mayuto mudogo… kimya kimya nilizunguka nyuma ya nyumba na mwezi huo unang’aa
nikaondoka nikaenda kutoka pale kijijini kwetu mpa nikafika Uvira. Muji wa
Uvira siujui na sina mtu ninaye mujua pale , lakini watu walikuwa wengi tena
wengi tu wanakwenda huko jua linakotoka wana sema kuna bahari lakini nyuma ya
bahari kuna watu wazuri sana. Ah Bwana nilijiunga na watu hao wanaokimbia Mayi
Mayi namie namkimbia Mayuto , lakini
jina langi ni Mayuto kama Babu.
Huko jama
zangu katika kijiwe hicho niliwaambia hata jua likitoka magharibi kwenda Mashariki
siwaambii kijiji changu najua kipo na watu wapo na wanajua kuwa walipotelewa na
mtoto… najua wapo na huko sirudi
ntakwenda tabora na ntaka
Ulyankulu au Pangale.
Mtu huyo
yupo hapa Tanzania na anauwezo wa
kuzungumza zaidi ya Lugha saba kwa ufasaha kabisa, lakini wewe muulize anaitwa
nani hapo utakuwa umezuwa ugomvi na ataondoka
bila kuaga.
Hivyo ukiwa
Kongo usivunge kuungua ….
No comments:
Post a Comment