Dar es salaam
Septemba Mosi ni siku ambayo kwa jiji la Dar es Salaam,
licha ya hali ya hewa kuwa na mawingu, maelfu ya watu walishuhudia kupatwa kwa
juwa na hali kuwa kama vile jua japo
lipo lakini halina nguvu wala mwanga wake hauna nguvu kama.
KUPATWA KWA JUA MBARALI-MBEYA
Hali hiyo ilisababisha watu kuingiwa hofu na kujiuliza kuna
nini kwasababu hali ya kukamatwa jua au
kupatwa kwa mwezi si jambo la kawaida.
Kwa hapa Dar es Salaam mwaka 1976 jua lilipatwa saa za asubuhi na mji ukawa umeingia mzizimo, watu waliingia
kubishana kwa nini imetokea wengine walisema ni kwa sababu Mohammad Ali –
Cacius Clay alikuwa kamtwanga mangumi
mpinzani wake George Foreman huko Manila
– The Manila Chila.
Ama kwa tukio la Septemba Mosi 2016, kilichoonekana ni kuwa
Waislamu waliita kwa ajili ya sala na waliingia misikitini na kusali, maelezo
ni kuwa, Walikuwa wanatukuza Uungu waMwenyezi Mungu”
“Mwaliona jua lilivyo kuwa na ukali wa joto ulivyo leo licha
ya kuwepo lakinilinaonekana kuwa li
baridi” alisikika Imam wa msikiti mmoja hapo Magomeni Mapipa. Walisimama kuswali mpaka jua lilipo kuwa tena
limerudia hali yake ya kawaida na tayari swala ya Adhuhuri ilikuwa
imeingia na watu waliunganisha nakuswali
hiyo swala ambayo huiswali kila siku nyakati hizo.
Hali ya kukamatwa jua na kutokea kuwa gubi gumbi kabisa
ilitokea Novemba Mosi mwaka 1948. Hizo ni taarifa ambazo ni kwa mujibu wa NASA
chombo ambacho ni huko Marekani, ambacho kimejaza mabingwa wa mambo ya anga na
hali za hewa. Hao ndio walipeleka timu ya watu kwenda kutua mwezini.
Wakati wa kukamatwa jua unatofautiana kuna sehemu ambazo ilikuwa ni sehemu kidogo
ambapo kivuli cha mwezi kiliangukia ardhini na hiyo ndiyo hali iliyotokea
jijini Dar es Salaam. Na sehemu zingine kama kule Njombe hali ilikuwa ni kuwa
kufunikwa kabisa; licha ya kuwa ni mchana lakini hakuna jua wala athari yake
haikuonekana.
Wakati Waislamu wanasema
wanasimama kuswali kumtukuza Mungu kwa
utukufu wake, kuna taarifa
zinazoeleza kuwa watu wa dini zingine kama wapagani wao walichukua ngoma
na kuanza kupiga ngoma zao ili kulitisha lile mzuka lililo gubika jua liondoke
na kuliachia jua katika hali yake.
Udadisiwetu haukwenda ndani zaidi, lakini kuna matukio
kadhaa yaliyotokea kama kule Sinza
karibu na mabwalo ya Lulu na
Utoji kuna madibwi ya maji na vijana walizunguka madimbwi hayo na kuangalia
hali hiyo, wanasema kwa kutumia kivuli cha jua ndani ya maji haina athari kwa
macho kama mtu akiangalia moja kwa moja
angani.
Watu wengine ambao
walikuwa karibu na mafundi wa welding, walitumia kile kioo ambacho hutumika kwa
kuchomelea vyuma, na ikawa ni deal ya kukodishwa watu kwa dakika moja moja na yulemtu aliyesimamia zoezi hilo inasemekana
kaondoka na kiasi cha mboga. Kila kichwa(mtu) ilikuwa shilingi mia mbili (200/=)
Katika kituo kimoja cha
mabazi sehemu ya mapipa,
walisikika, watu wakisema kuwa je hali hiyo
wanasayansi hawawezi kuingilia kati na kuizuwia ili kupunguza hofu kwa watu?
“Ah Bwana wana
Sayansi wanasoma hali ya kitu kilivyo na wanaweza kujaribu kuelezea tu
lakini wajaribu kuepusha jua lisipatwe
na mwezi au mwezi usipatwe na jua, hajatokea mbishi wanamna hiyo na hatatokea
mpaka mwisho wa dunia!
Lakini yule mdadisi aliendelea kusema mbona wamepiga hatua
mpaka wameumba kondoo wao wenyewe na hivi sasa wanaweza kuunda mimba nje ya
mimba na kuiitia tumboni mwa mwanamke
ambaye ni mgumba?”
“Astaghfirullahi! Enhe ndio wamefika kuumba ili nao
waabudiwe? Sikiliza bwana Hakuna anaweza kuunda manii wala yai la
mwanamke jinsi vilivyo hivi vitu
watachukua na kujaribu tu, lakini Hakuna uunga wala uunmbaji wamwogope Mola
wao. Firauni alidai kuwa yu Mungu na kusema alikuwa anapitisha mito naalikuwa
ana mabustani nchini kwake … na yalimfika yaliyo mfika maji hayo hayo aliyokuwa anajifanya Ndiyo
neema zake yalimwangamiza alipojaribu kumfuata Musa ili amwuue. Bwana we
wanaweza kujaribu kutabiri lini hayo yatatokea lakini kuyazuwiya ni Ng’odo!”
PICHA ZIFUATAZO ZINAONYESHA KUPATWA KWA JUA MBARALI-MBEYA
PICHA ZIFUATAZO ZINAONYESHA KUPATWA KWA JUA MBARALI-MBEYA
WATU WAKIANGALIA KUPATWA KWA JUA KUPITIA KIFAA MAALUMU
No comments:
Post a Comment